AM ZE GCR

Wednesday, August 13, 2014

WANAHARAKATI WALIVYOIPANIA BIRTHDAY YA YESU OKOA MITAA 24TH AUGUST 2014

Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii,bhasi bila shaka umekutana  na hili,wanaharakati wengi wa mziki wa Injili hususani wanaHipHop kwa kitambo sasa wamekuwa wakizungumzia  maadhimisho yanayosadikika kuwa ni makubwa kuwahi kutokea kwenye mziki wa Gospel Hiphop Tanzania,ambapo mtandao mkubwa wa harakati wa mziki  huo YESU Okoa Mitaa-YOM unatarajia kutimiza mwaka mmoja.
Kimsingi YOM imeshatimiza mwaka mmoja toka kuzinduliwa kwake kwa mara ya kwanza tar 28 july 2013,lakini kutokana na mishe za maisha mahadhimisho ya birthday yatafanyika tarehe 24/8/2014 katika kanisa la Dar Calvary Temple,Tabata kwa Mchungaji Ron Swai ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God,Tanzania.
Katika shamlashamla hizo wanaharakati wameonyesha jinsi gani walivyoipania siku hiyo adhimu,pengine kwa kuwa matamasha hayo hufanyika kwa nadra,wanaharakati wengi wiki hii wameaachia mawe mapya redioni au kwa mtandao ambapo kila mmoja ana mpango wa kufanya perfomance ya kwanza ya nyimbo yake siku hiyo,sipati picha.
RUNGU LA YESU
Ukianza na Rungu la Yesu ameachia ILIKUWA ZAMANI,ambayo alianza kuupa promo ujio huo toka mwanzoni  wa mwezi julai.
MARTIN BASHANDO
Martin Bashando pia ameachia ngoma yake ya WAHESHIMU WAZAZI,ambayo licha ya kuwa tu mtandaoni inaruka redioni sambaba na kazi ya Rungu la  Yesu .
BRIAN MWIMBA NA MCHUMBA WAKE
Brian Mwimba naye licha ya kuwa na mahangahiko na mambo ya harusi yake ambapo alitangaza uchumba wiki moja tu iliyopita hakutaka kuachwa nyuma kwa jinsi alivyopania sikukukuu hiyo na katika hali ya kushangaza Bishop Nickodemus Shaboka naye ameaamua kuvunja ukimya wake wa muda mrefu kwenye mziki wa hiphop baada ya kuwa busy na huduma ya kuhubiri na majukumu mapya ya ndoa,ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la UNISIKIE.
Bishop Nicko Shaboka na Mkewe
Ukiingia kwa mtandao ndio kumechafuka usipime ni habari ya mjini kila kona.
Changamoto ninayoiona hapa kwa Yesu Okoa Mitaa ni kuweza kufanya tamasha la kiwango kikubwa litakaloendana na promo zinazoendele,mimi mwenyewe sijui itakuaje...ngoja tuoneee
Cha msingi ni kuhudhuria DCT Tabata 24/08/2014
 

Tuesday, August 12, 2014

SAMWELI SASALI:MKE MWEMA ANATOKAJE KWA BWANA?!KWA BWANA NDO WAPI?!! KWANI KUOA BRAND NEW LAZIMA?KUPATA USED JE?

Katika pitapita zangu za facebook leo nimekutana na post iliyonyaka usikivu wangu kwa muda kutokana na umuhimu pamoja na utata wake baina  ya vijana wengi hasa kwa sisi tunaojulikana kama walokole,naomba ku share jambo hili kwa ku copy na kupaste  kutoka katika ukurasa wa Samweli Sasali,mtaangazaji  wa Chomoza ya CloudsTv,.....KAZI NI KWAKO


"Ni kweli kabisa Mungu ndiye atupaye mke na Mume lakini ni jukumu letu "Kujichagulia" waliojazana kwa Bwana. Kwani we unaelewaje Ukiambiwa Mitumba Mizuri Inapatikana Karume?au ukiambiwa Mitumba mizuri inapatikana Mwanjelwa?Ukifika Mwanjelwa ni jukumu lako kutafuta mitumba mizuri wewe kichwani kwako unajua Mitumba mizuri inapatikana Mwanjelwa full stop. Ama Ukiambiwa Mikopo Mizuri inapatikana Access Bank...ni jukumu lako kwenda branch yoyote ya Access Bank unaendelea na taratibu za mkopo.
Anayeanzisha Process za Kukopa ama kununua ngua no muhitaji. Sasa wewe kama unadhani Bwana ni Mmachinga unataka akuletee nyumbani utasubiri sana kwa Bwana ni kupana sana. Sawa sawa ukiambiwa nguo rahisi ziko Kariakoo. Kazi ni kwako kama ni Congo, Msimbazi, Kitumbini ama Kariakoo shimoni. Sasa wewe jifanye huelewe kuwa Mke mwema anapatikana kwa Bwana sasa unasubiria. Kwa Bwana ulisikia ni Mbinguni ama Kanisani kwenu tu?Kwa Bwana ni Kupana sana, ukiwa na akili ya kudhani kwa Bwana ni kwenu tu utazeeekea hapo. Zamani tulikuwa tunamsemo "Tembea Mungu akuone". Wachache sana wamewahi letewa nguo nyumbani.
Kwa kadri unavyoli Position duka lako linaweza sababisha ukawa na wateja ama huna wateja. Kuna tofauti kubwa sana ya bei kati ya fremu za barabarani za zile zilizo mbali ya barabara. Kuna wengine manijificha fichaaa mnajiweka mbaliii wakati ni wahitaji. Kuna wengine hamuonekani kabisa. Unakuta mdada anajifanya busy. Ibada ikiisha tu kapanda kagari kake. Unakuta ofisini ukitoka tu huna story na watu. Kwa taarifa yako Zakayo asingepanda Juu ya Mti Yesu asingemuona, Batimayo angelala nyumbani asingepiga kelele asinge tolewa upofu. Kuna wengine wanajifanya expensive sana kumbe ni wahitaji wakubwaaa halafu wanalalamika Mungu Mbona haunioni, mbona wenzangu wanaolewa. Jiulize tu "Unaonekana"?kwa taarifa yako dont quote me wrong duka kuwa barabarani halimaanishi lina vitu bei rahisi. Hujawahi sikia watu wanatoka Bunju kwenda Kariakoo kufanya shopping?
Kuna raha yake mdada kupigiwa goti na mkaka. Kuna raha yake pale unapoibua pamba kaliiii ya mtumba katikati ya mitumba mingi katika sagula sagula. Kuna raha yake unapochagua nguo uitakayo. Kuna watu mnajifanya hamtaki kuolewa na wakaka "used" ama "mdada" used. Utasikia aaah mie ntaolewa ama ntaoa kitu Brand New. Ndugu yangu hujapenda wewe. Ina maana una mashaka na Bwana?kuwa kuna wengine amewasafisha kwa damu yake na wengine amewasafisha dhambi zao kwa OMO?Ukinunua mtumba ukaufua vizuriii, ukauweka vile unataka kuna mtu ataujua umevaa nguo used?sii mpaka uanze kuongea mwenyewe?Kwa Bwana kuna Mabikira na Kwa Bwana pia wapo ambao sio Mabikira, kuna ma handsome na madungayembe wote wamejaa kazi kwako. Wewe Jifanye kuchagua chagua unataka kitu Brand New....Sasa najiulizaga swali Mkaka Unataka Brand New wakati Kanisani kwenu Kudungunyuana ni Dhambi kubwaaa tofauti na wale wengine ambao wao kupasha kiporo moto sio issue unakula jana kesho unapsha kidogo halafu unaendelea, yaani wanazundua albam kabisa kisha ndo wanaingia studio Kurekodi. Kwa ngoma inavyokatazwa kuzindua na unataka Brand New utajuaje?sii atakuambia mie Brand New....ukifika kule ni used utamuacha?Bwana anajua akufaaye unaweza ukapata kitu Brand New halafu mtoto wa watu full Kiburi. Kuna mambo tuu Mwachie Mungu. Akikupa Brand New Mshukuru, Akikupa sio Brand New kwa mtazamo wako Pia Mshukuru Maana anakuwazia Mema. Kwani ulisikia kuna barabara inakataza kupita Used Car?
ONYO: KAMA MKE MWEMA AMA MUME MWEMA ANAPATIKANA KWA BWANA HAIMAANISHI YEYOTE. HATA KAMA MITUMBA BEI RAHISI IKO KARIAKOO HUWA HATUNUNUI WOWOTE.
Amini amini nawaambia nalisema nanyi kwa Lugha ya kwenu kabisa ili niweze kueleweka. Kama Kwa "Bwana" Hupajui sema uambiwe. Haimaanishi ukifika Kariakoo unaweza usipotee. Ukipotea unauliza kwanza usije kutokomea kwenye Upotevu."

Monday, August 11, 2014

SECKOND CHAYNCE; MWANA GOSPEL HIPHOP ALIYEMDISS EMINEM KWA KUJIITA RAP GOD

Katika pitapita za mtandaoni siku moja nilikutana na video lyrics ifuatayo na ikanifanya nivutiwe kuangalia sio mbaya na wewe ukicheki kwanza

    
mwanzoni mwa mwaka huu moja kati ya rappers wakali duniani Eminem aliachia album yake ya sita inayokwenda kwa jina la  MMLP2,ambapo moja kati ya vibao alivovichia ni rap god "am starting to feel am rap god" unasema moja kati ya mistari kwenye nyimbo hiyo,sijajua kabisa alikua anamaanisha nini labda ni majigambo tu ya rap.
lakini jambo hilo halikuchukuliwa poa na rapper seckond chaynce moja kati ya waanzilishi wa kwanza wa kundi la HGA(His Glory Alone) akiwa na KB ambaye sasa yupo chini ya Reach Record inayomilikiwa na rapper Lecrae.
"i had a vision it was more than a dream,i saw the idols crushed under his feet"  anaanza seckond chaynce ambapo ametumia sauti,flow na mdundo unaofanana na ule wa Em kwenye rapgod.
hapa anatoa onyo kwa wale wanaojiita rap gods,sio kwa Em tu bali hata rappers wengine kama Jigga,Kanye na wengine wanapendelea kujiita majina yanayofanana na majina ya Mungu.
Chaynce amewapa maonyo makali katika mistari mingine inayofuata akiwaambia kitachowapata ni kama kilichompata yuda bila kuachia diss ya moja kwa moja aliyoirusha kwenye verse ya pili
Yo, If you're the rap god, call me chizzle the god killer
Though go-rilla, my God's illa than godzilla
Ipod filla psychotic coming hard as a charging rhinoceros
Never stop till my God give the relax chizzle
Hapa Chaynce anajifagilia kwamba kama wao ni miungu ya rap basi yeye ni god killer akimaanisha atawaua yani hawamuezi,pia anaendelea kwa kujitambulisha katika mistari inayofuata kuwa yeye amekuja kuwakilisha kweli.
katika kumalizia yote Chaynce anasema bila kujali anawaombea wote kuanzia Eminem,jay z,kanye na kila msanii mwenye nyendo kama hao jamaa kama nilivyomnukuu
 Reprobate looking boys
Eminem, Kanye West, Jay Z, y'all pray from them boys
And any other artist that is following the pattern of the devil
Tell em Christ made a way for them boys
Reconciliation with the father in heaven so they can be saved
Cos Christ is the way for them boys
Repent and turn away from your sins, Jesus Christ trust him
Man that's all I gotta say to them boys
kwa haraka unaweza sema jamaa kama anataka bifu na washikaji vilee..lakini kwa mtazamo wangu jamaa ka show love ya kutosha saana akionyesha jinsi gani gani anawakubali kile wanachofanya kama wasanii wa hiphop ndo maana amerap katika flow ile ile ya Em kitu ambacho si rahisi maana flow yenyewe imepinda kichizi ila tu alikuwa anataka kuwaweka sawa kimtamzamo kwa jinsi wanavyotakiwa kumchulia MUNGU

Wednesday, August 6, 2014

STORY NYUMA YA WIMBO WA "ILIKUWA ZAMANI" WA RUNGU LA YESU

    "kama mapenzi ilikuwa zamaani,sasa niko na mwokozi maisha ya dhambi siwezi"
maneno hayo yanasikika kwenye chorus ya joint mpya ya rapa mkali kutoka Yesu Okoa Mitaa,Rungu la Yesu iliyoimbwa kwa ustadi wa hali ya juu na bishop Nickodemus ikihashiria hisia za mapenzi zilizofika mwisho baada ya kuanza maisha mapya ndani ya kristo.
Ngoma hyo ilioachiwa mapema wiki hii katika media mbalimbali ikiwemo mitando ya kijamii imebeba story ya mapenzi ya kusisimua  ambayo ilinipa shauku kupiga story na Rungu la Yesu  ili atueleze kisa hicho ni cha kweli au ni sanaa tuu...
           Nilipoanza kumuuliza maswali Rungu alikuwa akiruka huku na kule ili kukwepa maswali yangu lakini  nilipombana kwa mtazamo wake binafsi anaichukuliaje nyimbo hii alifunguka yafuatayo
"Kwanza kabisa nyimbo hii niliiandika miaka sita iliyopita,japo nimeirekodi na kuiachia hivi karibuni,pili  nyimbo hii imebeba mkasa ulionikuta punde tu nilipoamua kumpa Yesu maisha yangu" alifunguka Rungu la Yesu,ambapo alidai alikuwa na demu mkali ambaye yeye alikua anamzimia balaa,na alipookoka alikuwa  hajui namna ambayo ataweza kuachana na mrembo yule kwa kuwa alimpenda saana jambo ambalo lilikuwa linampa mawazo sana,inawezekanaje kijana kuyashinda mambo hayo?
 Rungu anasema jambo hilo lilikuwa mtihani kwake mpaka pale siku moja alipokuwa akiwaza kuhusu jambo hilo alisikia sauti ya Yesu Kristo ikimwambia ndani," MIMI PIA NILIKUWA MWANADAMU LAKINI NILIYASHINDA HAYO "pia sauti hiyo iliendelea kwa kumwambia kuwa akishinda jaribu hilo basi atampatia mke mzuri zaidi,ndipo hapo Rungu alipata ujasiri wa kumtema yule binti na anashukuru Mungu yule binti aliweza kumwelewa baada ya kuweka wazi ya kuwa ameokoka
Nilipomuuliza Rungu ana ushauri gani kwa vijana waliokwama eneo kama hili alifunguka na kusema  "tunaweza kudhani tuna vitu vizuri,lakin Mungu anavyo vizuri zaidi vya kutupa,kama unahisi unashindwa kabisa tafuta ushauri kwa wachungaji na watu wenye ufahamu zaidi wakusaidie,yote yanawezekana kwa Mungu"
Mwisho wa yote Rungu aliwaomba watu wote wanaompenda kuendelea kumsapoti ikiwemo na kujitokeza kwa wingi siku ya  jumapili ya tarehe 24/08/2014 kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja toka kuanzishwa kwa Yesu Okoa Mitaa,ambapo kwa mara ya kwanza atachombeza kibao hicho kipya jukwaani sambamba na Brian Mwimba ambae pia atatambulisha ngoma yake mpya ya Bomoa Bomoa..
Bonyeza hapa kusikiliza ILIKUWA ZAMANI

Saturday, June 21, 2014

A SONG TO DEDICATE TO YOUR LOVER/SPOUSE?

SONG:BUTTONS
ARTIST:LECRAE
ALBUM:GRAVITY
CHECK IT HERE:BUTTONS



For better or for worse
Make it work
I ain't goin nowhere

[Verse 1:]
Yeah, I messed up, but you hurt me, blew it like it's yo birthday
And you love it baby on Wednesday, but I make you sick on Thursday
And I know I'm wrong and you shuttin' down, and I touch down like "What now?"
Why we going through all this? Why things gotta be rough now?
But, you had so many break-ups, you can't believe
You go and break my heart that I forgive and I ain't leave
Don't define you by your faults, ain't gon' push your buttons either
Everyday we startin' fresh, this is how it's s'posed to be
Never try to take advantage, you respect me as a man
But every once awhile you get to poppin' off and say stuff you shouldn't be sayin'
But I'm with you, I ain't playin', if it's thick or if it's thin
Both the times and your figure, girl, this is who I am
I love you baby, that's real talk, and this life we live is a real walk
I ain't goin' nowhere, tell your girlfriends that it's still on
I love you baby, that's real talk, this life we live is a real walk
I ain't goin' nowhere, tell your friends that it's on

[Hook:]
For better or for worse
Sometimes I make you sick, and you get on my nerves
Make it work
I ain't goin' nowhere, and I give you my word
I'm a be right here
So though push my buttons
I ain't leavin'
You can keep on pushin'
I ain't leavin'

[Verse 2:]
I be makin' you mad, girl
But you said you'll never leave me lonely
So I had to put a ring up on it, cause our commitment ain't no game
Yeah we laugh, but we ain't playin', I'm a always be yo mane
And I know sometimes I upset you, be pushin' all yo buttons
We be fussin', fighting over nothin', you can try to leave, but I'm comin'
We gon' work it out with no runnin', pushin', shovin'
I know sometimes that I'm selfish, but I jump in front of yo' bullet
Cause you everything that prayed for, plus a little bit extra
Even when you getchu' an attitude and you act a little bit extra
Listen, you make me better, babe, you make me better, babe
You got my heart and you can have it for forever, baby
And though we'll never break up, I hate it when we mad
But love it when we get to make up, no lines that I could make up
To let you know how much I got you covered, girl
And I only be pushin' yo buttons because I love you, girl

[Hook]
 

Wednesday, June 18, 2014

RUNGU LA YESU KAMTOSA DEMU WAKE?

   Si rahisi kumjua mtu  kwa siku moja,watu wengi tunaodhani tunawajua,si kweli kwamba tunawajua sana,ila kadiri ya unavyokaa na mtu ndivyo unavyojua kiundani,yaani mienendo na tabia
       Watu wengi tunaujua upande mmoja wa rappa mahiri kabisa katika tasnia nzima ya muziki wa injili,Rungu la Yesu.
Bila shaka wengi tunamuheshimu huyu jamaa kwa kile ambacho amekifanya na anakifanya sasa katika tasnia hii,harakati za Yesu Okoa Mitaa,Matasha,Semina na ishu mbalimbali zinazohusu kuupaisha ufalme wa Yehova.
       Lakini umeshawai kujiuliza upande wa pili wa maisha wa kijana huyu ambaye anatikisa mawimbi ya redio nyingi za gospel kwa hits kali?kila mmoja anapita au amewahi kupita sehemu fulani kwenye maisha ambayo imempa changamoto ya kutobaki kama vile alivyo.
     Kwa namna moja au nyingine nipo karibu na huyu jamaa kama mmoja wa watu wanao support Yesu Okoa Mitaa (YOM project Tz),ila ukaribu huo haimaanishi kwamba naweza kujua kila kitu kitu kuhusu yeye..


Mpaka naiona video hii,bado siwezi kusema mambo yaliyoongelewa humu ni kweli,uongo au saanaa tu,ila nashawishika kumtafuta rungu ili nichonge nae kuhusu hayo maneno ya kwenye video hasa pale hii kitu itapokuwa rasmi.
Ni kweli alimtosa huyu binti?Ni kweli hawapo tena,au ndo chini ya carpet?
Anamaanisha anachosema? ana ushauri gani kwa jina wanaopita hapo?
kwa sasa sina majibu ila nadhani majibu yatakuwa hewani very soon..




Friday, June 21, 2013

HAINA UTATA; UZINDUZI WA ALBAMU YA RUNGU LA YESU MWEZI WA SABA

Rungu la Yesu,mwenye shati la purple
Baada ya tetesi nyingi mtandaoni kuhusiana na uzinduzi wa Rapper anaezitikisa ngome za shetani,Rungu la Yesu amethibitisha kuwa uzinduzi utakuwa ni tarehe 28/7/2013  katika kanisa la dar es salaam calvary temple,tabata shule,
        Katika mtandao wa facebook Rungu ameliongelea sana swala hili pamoja na kukusanya maoni kutoka kwa mashabiki wake juu ya uzinduzi huo.
Rungu la Yesu atazindua album ya video inayokwenda kwa jina la AMANI YA BWANA.kumbuka ni tarehe 28/7/2013..