AM ZE GCR

Wednesday, June 18, 2014

RUNGU LA YESU KAMTOSA DEMU WAKE?

   Si rahisi kumjua mtu  kwa siku moja,watu wengi tunaodhani tunawajua,si kweli kwamba tunawajua sana,ila kadiri ya unavyokaa na mtu ndivyo unavyojua kiundani,yaani mienendo na tabia
       Watu wengi tunaujua upande mmoja wa rappa mahiri kabisa katika tasnia nzima ya muziki wa injili,Rungu la Yesu.
Bila shaka wengi tunamuheshimu huyu jamaa kwa kile ambacho amekifanya na anakifanya sasa katika tasnia hii,harakati za Yesu Okoa Mitaa,Matasha,Semina na ishu mbalimbali zinazohusu kuupaisha ufalme wa Yehova.
       Lakini umeshawai kujiuliza upande wa pili wa maisha wa kijana huyu ambaye anatikisa mawimbi ya redio nyingi za gospel kwa hits kali?kila mmoja anapita au amewahi kupita sehemu fulani kwenye maisha ambayo imempa changamoto ya kutobaki kama vile alivyo.
     Kwa namna moja au nyingine nipo karibu na huyu jamaa kama mmoja wa watu wanao support Yesu Okoa Mitaa (YOM project Tz),ila ukaribu huo haimaanishi kwamba naweza kujua kila kitu kitu kuhusu yeye..


Mpaka naiona video hii,bado siwezi kusema mambo yaliyoongelewa humu ni kweli,uongo au saanaa tu,ila nashawishika kumtafuta rungu ili nichonge nae kuhusu hayo maneno ya kwenye video hasa pale hii kitu itapokuwa rasmi.
Ni kweli alimtosa huyu binti?Ni kweli hawapo tena,au ndo chini ya carpet?
Anamaanisha anachosema? ana ushauri gani kwa jina wanaopita hapo?
kwa sasa sina majibu ila nadhani majibu yatakuwa hewani very soon..




1 comment:

  1. Yeeeeeah, Umempakitu poa nazani dada kakuelewa, uliahidi utamuoa lakini leo kageuka doa, duh!!!! saana tu. hhaahahahaaa.

    Kama mapeeeeeenzi!!!!!!

    ReplyDelete