AM ZE GCR

Wednesday, May 15, 2013

MANENO KUNTU.....KUTOKA KWA COMEDIAN CHAVALA,....NI MARUFUKU!!ku do the following



                                                     #......NI MARUFUKU!!##
               Ni marufuku kwa kijana yeyote wa kiume yule mwenye akili timamu na kiasi cha utu ndani yake kumwambia kila msichana ANAMPENDA,hali hamaanishi kwa maneno hayo asemayo....kuna tofauti kubwa sana ya kupenda na kutamani,ukisoma 1 kor 13 ndio utajua kweli unapenda au umemtamani tu sijui nini alichonacho(unajua mwenyewe),sasa ikiwa binti yuko single na wewe unaropoka maneno hayo,unamfanya awe attention na wewe na hata serious opportunity zikampita na mara wewe unachepuka na kumuachia maumivu,ambayo yanakuja kuwagharimu wajao maana walipia care etra kwa maumivu uliyosababisha!
Be serious,huwezi kuwa na kila mtu hata kama wewe ni "suleiman" kiasi gani!!


              ANGALIZO; Inawezekana kuwa na urafiki wa kawaida kati ya msiichana na mvulana bila shida yeyote ile,yaani kaka na dada,lakini nashangaa watu wengi wakiwa karibu tu kitu kinachoinuka ni tamaa,why?
Na nimegundua kuwa kinachowagharimu wengi ni UONGO,yaani ukikutana na mtu basi unataka ujitambulishe kwa kujikweza ili aone wewe ndio mmh kumbe hamna kitu,but once you become honest,you will be very real and you will enjoy your life!!
INGAWA PIA KUNA WASICHANA AMBAO WANAPENDA SANA KUDANGANYWA,YAANI UKIMWAMBIA UKWELI ANAKUKASIRIKIA,ILA UKIMDANGANYA ANACHEKELEA,Be careful kama unampenda kijana usidhani ukijirahisi ndio atakuheshimu,atakupitia na ataenda zake....HEY LADIES PUT VALUE ON YOURSELF!!!!
Hey guys nimesema marufuku,tena nasema marufuku,sasa endeleeni tu!!!!......mtavuna kila mpandacho na hata kama si leo basi mjiandae na binti zenu kufanyiwa vivyo hivyo!!!!