AM ZE GCR

Tuesday, August 12, 2014

SAMWELI SASALI:MKE MWEMA ANATOKAJE KWA BWANA?!KWA BWANA NDO WAPI?!! KWANI KUOA BRAND NEW LAZIMA?KUPATA USED JE?

Katika pitapita zangu za facebook leo nimekutana na post iliyonyaka usikivu wangu kwa muda kutokana na umuhimu pamoja na utata wake baina  ya vijana wengi hasa kwa sisi tunaojulikana kama walokole,naomba ku share jambo hili kwa ku copy na kupaste  kutoka katika ukurasa wa Samweli Sasali,mtaangazaji  wa Chomoza ya CloudsTv,.....KAZI NI KWAKO


"Ni kweli kabisa Mungu ndiye atupaye mke na Mume lakini ni jukumu letu "Kujichagulia" waliojazana kwa Bwana. Kwani we unaelewaje Ukiambiwa Mitumba Mizuri Inapatikana Karume?au ukiambiwa Mitumba mizuri inapatikana Mwanjelwa?Ukifika Mwanjelwa ni jukumu lako kutafuta mitumba mizuri wewe kichwani kwako unajua Mitumba mizuri inapatikana Mwanjelwa full stop. Ama Ukiambiwa Mikopo Mizuri inapatikana Access Bank...ni jukumu lako kwenda branch yoyote ya Access Bank unaendelea na taratibu za mkopo.
Anayeanzisha Process za Kukopa ama kununua ngua no muhitaji. Sasa wewe kama unadhani Bwana ni Mmachinga unataka akuletee nyumbani utasubiri sana kwa Bwana ni kupana sana. Sawa sawa ukiambiwa nguo rahisi ziko Kariakoo. Kazi ni kwako kama ni Congo, Msimbazi, Kitumbini ama Kariakoo shimoni. Sasa wewe jifanye huelewe kuwa Mke mwema anapatikana kwa Bwana sasa unasubiria. Kwa Bwana ulisikia ni Mbinguni ama Kanisani kwenu tu?Kwa Bwana ni Kupana sana, ukiwa na akili ya kudhani kwa Bwana ni kwenu tu utazeeekea hapo. Zamani tulikuwa tunamsemo "Tembea Mungu akuone". Wachache sana wamewahi letewa nguo nyumbani.
Kwa kadri unavyoli Position duka lako linaweza sababisha ukawa na wateja ama huna wateja. Kuna tofauti kubwa sana ya bei kati ya fremu za barabarani za zile zilizo mbali ya barabara. Kuna wengine manijificha fichaaa mnajiweka mbaliii wakati ni wahitaji. Kuna wengine hamuonekani kabisa. Unakuta mdada anajifanya busy. Ibada ikiisha tu kapanda kagari kake. Unakuta ofisini ukitoka tu huna story na watu. Kwa taarifa yako Zakayo asingepanda Juu ya Mti Yesu asingemuona, Batimayo angelala nyumbani asingepiga kelele asinge tolewa upofu. Kuna wengine wanajifanya expensive sana kumbe ni wahitaji wakubwaaa halafu wanalalamika Mungu Mbona haunioni, mbona wenzangu wanaolewa. Jiulize tu "Unaonekana"?kwa taarifa yako dont quote me wrong duka kuwa barabarani halimaanishi lina vitu bei rahisi. Hujawahi sikia watu wanatoka Bunju kwenda Kariakoo kufanya shopping?
Kuna raha yake mdada kupigiwa goti na mkaka. Kuna raha yake pale unapoibua pamba kaliiii ya mtumba katikati ya mitumba mingi katika sagula sagula. Kuna raha yake unapochagua nguo uitakayo. Kuna watu mnajifanya hamtaki kuolewa na wakaka "used" ama "mdada" used. Utasikia aaah mie ntaolewa ama ntaoa kitu Brand New. Ndugu yangu hujapenda wewe. Ina maana una mashaka na Bwana?kuwa kuna wengine amewasafisha kwa damu yake na wengine amewasafisha dhambi zao kwa OMO?Ukinunua mtumba ukaufua vizuriii, ukauweka vile unataka kuna mtu ataujua umevaa nguo used?sii mpaka uanze kuongea mwenyewe?Kwa Bwana kuna Mabikira na Kwa Bwana pia wapo ambao sio Mabikira, kuna ma handsome na madungayembe wote wamejaa kazi kwako. Wewe Jifanye kuchagua chagua unataka kitu Brand New....Sasa najiulizaga swali Mkaka Unataka Brand New wakati Kanisani kwenu Kudungunyuana ni Dhambi kubwaaa tofauti na wale wengine ambao wao kupasha kiporo moto sio issue unakula jana kesho unapsha kidogo halafu unaendelea, yaani wanazundua albam kabisa kisha ndo wanaingia studio Kurekodi. Kwa ngoma inavyokatazwa kuzindua na unataka Brand New utajuaje?sii atakuambia mie Brand New....ukifika kule ni used utamuacha?Bwana anajua akufaaye unaweza ukapata kitu Brand New halafu mtoto wa watu full Kiburi. Kuna mambo tuu Mwachie Mungu. Akikupa Brand New Mshukuru, Akikupa sio Brand New kwa mtazamo wako Pia Mshukuru Maana anakuwazia Mema. Kwani ulisikia kuna barabara inakataza kupita Used Car?
ONYO: KAMA MKE MWEMA AMA MUME MWEMA ANAPATIKANA KWA BWANA HAIMAANISHI YEYOTE. HATA KAMA MITUMBA BEI RAHISI IKO KARIAKOO HUWA HATUNUNUI WOWOTE.
Amini amini nawaambia nalisema nanyi kwa Lugha ya kwenu kabisa ili niweze kueleweka. Kama Kwa "Bwana" Hupajui sema uambiwe. Haimaanishi ukifika Kariakoo unaweza usipotee. Ukipotea unauliza kwanza usije kutokomea kwenye Upotevu."

1 comment: