AM ZE GCR

Thursday, May 16, 2013

HATA UWE MBISHI VIPI,MWISHO WA SIKU UTASEMA TU "BWANA YESU ASIFIWE"

SONG:BWANA YESU ASIFIWE

ARTIST:RUNGU LA YESU

PRODUCTION;COMBINATION SOUND(MAN WATER)

kusikiliza wimbo nenda www.reverbnation.com/rungulayesuhiphop

CHORUS;

Nisiposema mimi Bwana Yesu asifiwe

yatainuka mawe yatasema asifiwex2

(sasa)......Bwana Yesu asifiwe!!

(woooote).....Bwana Yesu asifiwe

(twendeeee)...Bwana Yesu asifiweee!!

hata kama ni mbishi sema Yesu asifiwee!!!X2

verse 1. 

Bado me natangaza ya kuwa Yesu ni Bwana

hata yule shetani anajua Yesu ni Bwana

japo wengi mnabisha nawaona hamna maana

sababu mmefungwa mko chiini ya laana

anatenda mambo mengi Bwana Yesu ya kutisha

ndo mana anytime me napenda kumwakilisha

anaponya na magonjwa yale sugu yakutisha

jambo hili ni wazi rafiki usije bisha

hivi nani ndugu kafa tena kafufuka

siku ile ya tatu miamba ikapasuka

hata watatakatifu waliolala wakainuka 

mji ule mzuri mtakatifu wakafika

mikono juu rafiki ishara kwamba una surrender

bila kuwa na Yesu hakuna jambo utalotenda

alifufua maiti ya lazaro hadharani

muda wa siku nne iliyozikwa kaburini

iliyoanza oza harufu mpaka kunuka

lakini Bwana Yesu na uhai akamvika

Repeat chorus

verse II

Ni uzima Yesu yeye wa milele bado nasema

neno hili ni kweli litasimama

walikwepo wengi wengi manabii wameshakoma 

mitume na mitume wote hao wameshakoma

Yesu wangu ni shujaa haitaji yeye tetewa 

kwa marungu na mapanga Duuuh hiyo sawa

ulipuke na mabomu eti ujitoe muhanga 

si bora unywe soda tamu na kar anga

karibu Yesu wangu rafiki sema ni Bwana

alikuumba wewe na mimi weka bayana

kwake Yesu mwokozi ng'ang'ana weka dhamana

amini nakwambia mbinguni tutaonana

sasa simama hapo ulipo sema mwenyewe

sema Yesu ni Bwana asije Yesu kukana 

sema Yesu ni Bwana asije Yesu kukana

repeat chorus again

verse III

watu wote tambueni ya kwamba Yesu ni Bwana

iwe wanazuoni wapagani sema Bwana

ndani ya nyumba zote za ibada sema Bwana

Yesu ni jemedari wa vita Yesu ni bwana

Hi Tanzania Kenya Uganda inafana

Rungu nafarijika mnapokiri Yesu Bwana

kwa mikito mizito hiphop raga mnanena

kumtangaza Yesu kama zangina zangina

mimi Rungu la Yesu kitambo namkiri Bwana

nipo tayari kufa sababu Yesu ni Bwana

siogopi mizinga na matukano bunduki

wala vitisho vyenu na chuki hizo za chuki

nitamwamini Bwana na kumsifu siku zote

kwa mali zangu vyote viungo vyangu yani vyote

mtambue mwenzenu nampenda moyo wote

nawe shetani wewe nakuponda siku zote

repeat chorus