Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii,bhasi bila shaka umekutana na hili,wanaharakati wengi wa mziki wa Injili hususani wanaHipHop kwa kitambo sasa wamekuwa wakizungumzia maadhimisho yanayosadikika kuwa ni makubwa kuwahi kutokea kwenye mziki wa Gospel Hiphop Tanzania,ambapo mtandao mkubwa wa harakati wa mziki huo YESU Okoa Mitaa-YOM unatarajia kutimiza mwaka mmoja.
Kimsingi YOM imeshatimiza mwaka mmoja toka kuzinduliwa kwake kwa mara ya kwanza tar 28 july 2013,lakini kutokana na mishe za maisha mahadhimisho ya birthday yatafanyika tarehe 24/8/2014 katika kanisa la Dar Calvary Temple,Tabata kwa Mchungaji Ron Swai ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God,Tanzania.
Katika shamlashamla hizo wanaharakati wameonyesha jinsi gani walivyoipania siku hiyo adhimu,pengine kwa kuwa matamasha hayo hufanyika kwa nadra,wanaharakati wengi wiki hii wameaachia mawe mapya redioni au kwa mtandao ambapo kila mmoja ana mpango wa kufanya perfomance ya kwanza ya nyimbo yake siku hiyo,sipati picha.
RUNGU LA YESU
Ukianza na Rungu la Yesu ameachia ILIKUWA ZAMANI,ambayo alianza kuupa promo ujio huo toka mwanzoni wa mwezi julai.
MARTIN BASHANDO
Martin Bashando pia ameachia ngoma yake ya WAHESHIMU WAZAZI,ambayo licha ya kuwa tu mtandaoni inaruka redioni sambaba na kazi ya Rungu la Yesu .
BRIAN MWIMBA NA MCHUMBA WAKE
Brian Mwimba naye licha ya kuwa na mahangahiko na mambo ya harusi yake ambapo alitangaza uchumba wiki moja tu iliyopita hakutaka kuachwa nyuma kwa jinsi alivyopania sikukukuu hiyo na katika hali ya kushangaza Bishop Nickodemus Shaboka naye ameaamua kuvunja ukimya wake wa muda mrefu kwenye mziki wa hiphop baada ya kuwa busy na huduma ya kuhubiri na majukumu mapya ya ndoa,ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la UNISIKIE.
Bishop Nicko Shaboka na Mkewe
Ukiingia kwa mtandao ndio kumechafuka usipime ni habari ya mjini kila kona.
Changamoto ninayoiona hapa kwa Yesu Okoa Mitaa ni kuweza kufanya tamasha la kiwango kikubwa litakaloendana na promo zinazoendele,mimi mwenyewe sijui itakuaje...ngoja tuoneee
Cha msingi ni kuhudhuria DCT Tabata 24/08/2014
No comments:
Post a Comment