AM ZE GCR

Wednesday, August 6, 2014

STORY NYUMA YA WIMBO WA "ILIKUWA ZAMANI" WA RUNGU LA YESU

    "kama mapenzi ilikuwa zamaani,sasa niko na mwokozi maisha ya dhambi siwezi"
maneno hayo yanasikika kwenye chorus ya joint mpya ya rapa mkali kutoka Yesu Okoa Mitaa,Rungu la Yesu iliyoimbwa kwa ustadi wa hali ya juu na bishop Nickodemus ikihashiria hisia za mapenzi zilizofika mwisho baada ya kuanza maisha mapya ndani ya kristo.
Ngoma hyo ilioachiwa mapema wiki hii katika media mbalimbali ikiwemo mitando ya kijamii imebeba story ya mapenzi ya kusisimua  ambayo ilinipa shauku kupiga story na Rungu la Yesu  ili atueleze kisa hicho ni cha kweli au ni sanaa tuu...
           Nilipoanza kumuuliza maswali Rungu alikuwa akiruka huku na kule ili kukwepa maswali yangu lakini  nilipombana kwa mtazamo wake binafsi anaichukuliaje nyimbo hii alifunguka yafuatayo
"Kwanza kabisa nyimbo hii niliiandika miaka sita iliyopita,japo nimeirekodi na kuiachia hivi karibuni,pili  nyimbo hii imebeba mkasa ulionikuta punde tu nilipoamua kumpa Yesu maisha yangu" alifunguka Rungu la Yesu,ambapo alidai alikuwa na demu mkali ambaye yeye alikua anamzimia balaa,na alipookoka alikuwa  hajui namna ambayo ataweza kuachana na mrembo yule kwa kuwa alimpenda saana jambo ambalo lilikuwa linampa mawazo sana,inawezekanaje kijana kuyashinda mambo hayo?
 Rungu anasema jambo hilo lilikuwa mtihani kwake mpaka pale siku moja alipokuwa akiwaza kuhusu jambo hilo alisikia sauti ya Yesu Kristo ikimwambia ndani," MIMI PIA NILIKUWA MWANADAMU LAKINI NILIYASHINDA HAYO "pia sauti hiyo iliendelea kwa kumwambia kuwa akishinda jaribu hilo basi atampatia mke mzuri zaidi,ndipo hapo Rungu alipata ujasiri wa kumtema yule binti na anashukuru Mungu yule binti aliweza kumwelewa baada ya kuweka wazi ya kuwa ameokoka
Nilipomuuliza Rungu ana ushauri gani kwa vijana waliokwama eneo kama hili alifunguka na kusema  "tunaweza kudhani tuna vitu vizuri,lakin Mungu anavyo vizuri zaidi vya kutupa,kama unahisi unashindwa kabisa tafuta ushauri kwa wachungaji na watu wenye ufahamu zaidi wakusaidie,yote yanawezekana kwa Mungu"
Mwisho wa yote Rungu aliwaomba watu wote wanaompenda kuendelea kumsapoti ikiwemo na kujitokeza kwa wingi siku ya  jumapili ya tarehe 24/08/2014 kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja toka kuanzishwa kwa Yesu Okoa Mitaa,ambapo kwa mara ya kwanza atachombeza kibao hicho kipya jukwaani sambamba na Brian Mwimba ambae pia atatambulisha ngoma yake mpya ya Bomoa Bomoa..
Bonyeza hapa kusikiliza ILIKUWA ZAMANI

No comments:

Post a Comment