AM ZE GCR

Wednesday, May 15, 2013

RUNGU LA YESU KUDONDOKA UNYAMWEZINI KABLA YA UZINDUZI

Kwa kile nilichokiita tetesi kuwa rapa mkali wa Gospel GEORGE RUNGU a.k.a RUNGU LA YESU amefunguka rasmi juu ya uzinduzi wa album yake ya video na kusema kwamba swala la uzinduzi ni kweli lipo lakini hakusema lini wala wapi.."Kiukweli uzinduzi upo na maandalizi yapo ila sitaki kutaja siku wala sehemu sababu bado nina mambo mengi hivi unavyoniona sijatulia kabisa maana mwisho wa mwezi huu nina semina pande za tabora huko ambayo ndio imenifanya kuwa busy ",alifunguka Rungu na kuendelea kusema kuwa  licha ya kwenda Tabora kihuduma pia atakwepo katika center moja ya watoto yatima akiwafundisha baadhi ya vitu kuhusu Hip Hop ..

"kwa hiyo unaweza kuona jinsi gani nilivokua busy,mana ntakuwa huko kuanzia
tarehe 28,sina uhakika bado ntarudi lini kwa hiyo baada ya kurudi Tabora ntajua hasa tarehe yangu ya kuzindua,nawaomba tu watu wanaoni support kuwa wavumilivu kidogo nawaomba tuwe pamoja katika maombi na maandalizi yote"alimalizia Rungu ambae pia anajiandaa kufanya mkutano wa injili Mbinga mkoani Ruvuma mwezi wa kumi...