JICHO LA TATU.....KIPIMO HALISI CHA MAFANIKIO YAKO,BY FARAJA MNDEME
SUCCESS & FAILURE.
1.Kuna kamtazamo fulani ambako watu wengi tunako kuhusu Mafaniko kwenye
maisha yetu ambako Muda mwingine kanatupoteza na kutufanya tukose
mwelekoo kwenye maisha yetu ya kila siku.
"Mafanikio kwenye
maisha sio yale ya kujilinganisha na mtu mwingine,Mafanikio ni hali ya
kuweza kufikia lengo fulani kwenye maisha au jambo lolote ambalo
umejiwekea.Mfano Ulipanga Upate Million 100 kwa Mwaka na Ukafanikiwa
Kupata Million 70 wewe umeshindwa haukufanikiwa kwenye lengo
Lako.Angalizo Unaweza ukawa umewapita watanzania wengi kupata milioni 70
kwa Mwaka lakini Ukilinganisha na Malengo yako ya Kupata Million 100
kwa Mwaka wewe bado umeshindwa kufikia lengo.
Kipimo cha Mafanikio kwenye Miasha sio Mtu Mwingine umemzidi Mara
ngapi.Kipimo Halisi cha Mafinikio ni wewe mwenyewe je Umefikia malengo
yako kiasi gani.Wewe ndio Kipimo cha mafikio yako Binafsi ingawa wengine
wanaweza kukuona Umefanikiwa
2.Kushindwa ni hali ya kutoweza
kufikia malengo fulani kwenye maisha wewe binafsi na sio kujilinganisha
na mwingine.Unaweza Ukawa unafanya vizuri kwenye jambo fulani lakini
ukilinganisha na uwezo ulio nao kulingana na wengine kumbe ungefanya
vizuri zaidi.Kushindwa kwenye jambo haitegemei umewapita watu mara ngapi
kwenye hiko kitu/jambo bali wewe umetimiza lengo lako wewe binafsi
kwenye malengo yako.Machoni Petu unaweza kuwa umefanikiwa lakini
Ukieenda kwenye ile idadi ya Malengo yako kumbe haujafanikiwa..Pia
machoni mwetu tunaweza kuona umeshindwa kumbe wewe ndio umefanikiwa
kufikia malengo yako kulingana na kpimo chako wewe Binafsi.Kushindwa
kufikia malengo fulani hakutegemei kujilinganisha na wengine.Wewe ndio
kipimo cha Kushindwa kwako juu ya jambo fulani.
....Kipimo
Halisi cha Mafanikio au Kushindwa ni Kile cha Kwako Binafsi
Ulichojiwekea kulingana na Uwezo uliokuwa nao na sio Kile ambacho
Unatumia kujilinganisha na wengine....
Tumeshaimaliza Robo ya kwanza ya Mwaka na ya Pili ndio Ipo Ukingoni ..jiulizee...
#Above The Limits#